Skip to main content

Pamoja na kuwa kwamba mazingira yanayozunguka eneo la ufugaji kuwa miongoni mwa vyanzo vya magonjwa kwa kuku, chakula cha kuku pia kimetajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu vya magonjwa kwa kuku wa mayai.  

Daktari wa mifugo kutoka Interchick Bwana Vincent Lukanima ameeleza hayo wakati akifafanua kuhusiana na magonjwa ya msimu kwa kuku wa mayai na namna ya kuwakinga dhidi ya magonjwa hayo ili kuepukana na vifo vya mara kwa mara na kuleta utagaji wenye tija kwa mfugaji.  

 Chakula bora cha kuku kilichozalishwa na kuhifadhiwa katika mazingira ya usafi, chenye virutubishi vya kutosha kulingana na mahitaji husika ya kuku wa mayai ili kumpa kuku afya bora na ukuaji stahiki kimekuwa nguzo muhimu katika afya kuku. Lishe bora kwa kuku inaimarisha mfumo wa kinga wa kuku hivyo kuongeza uwezo wa kuku kujikinga na magonjwa mbali mabli yakiwemo magonjwa ya msimu kama vile kideri. Utunzaji usio sahihi wa chakula cha kuku hunasababisha uwepo wa vimelea kama vile fangasi kwenye chakula ambao husababisha matatizo mbalimbali kwa kuku ikiwemo shida katika mfumo wa upumuaji kwa kuku.   

Hata hivyo si ubora na usafi wa chakula tu ndio unaoweza kuzuia mashambulizi ya magonjwa kwa kuku wa mayai, bali hata usafi wa vyombo vya chakula hicho pamoja na utolewaji wa chanjo husika kwa wakati sahihi kulingana na ushauri wa daktari wako wa mifugo unaotegemeana na mazingira ya eneo lako la ufugaji ndio hukamilisha usalama wa ukuaji wa kuku wako wa mayai wenye utagaji wa faida.

Leave a Reply